Posts

JUMA ABDUL ATAJA SABABU ZA KUONDOKA YANGA

Ndoto ya wachezaji wengi ni kucheza Simba na Yanga na baada ya hapo ndipo inaanza mipango ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Juma Abdul ameshacheza nchini kwa kiwango cha juu akiwa na klabu ya Yanga na kufanikiwa kuchaguliwa mchezaji bora wa ligi kuu Tnzania bara.       “Nawaza sana kuchezaja nje ya Tanzania na sio mimi pekeyangu, kuna wachezaji wengi ambao wana vipaji vya kucheza nje lakini changamoto imekuwa nafasi au mawakala wetu kuwachukuwa wachezaji kuwapeleka sehemu wafanye majaribio kuona kama wanaweza kufanikiwa. Wachezaji wenzetu wa Afrika Magharibi wanaamini kile wanachokiamini mchezaji anaweza kuwa hana hata kipaji lakini anaamini nikifika sehemu fulani nikifanya kazi nitafanikiwa”-Juma Abdul wakati anazungumza na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’.       “Kinachotukwamisha sisi waliotutangulia mwanzo kabisa hawakuweka njia nzuri mimi naamini hata Nigeria sasa hivi wachezaji wengi wanatoka kwenda kucheza Ulaya siyo kwamba ni wachezaji hatari lakini n...

HUYU NDIYE MRITHI WA KOCHA WA YANGA GEORGE LWANDAMINA,ATAIPA MATAJI YANGA NA PIA NI MWIBA KWA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Image
Uongozi wa Yanga umemtangaza atakaekaimu nafasi ya kocha mkuu iliyoachwa wazi na George Lwandamina ambaye katikati ya juma hili alirejea kwao na kuijiunga na klabu yake ya zamani ZESCO united. Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa uongozi wa Yanga umemwandika barua George Lwandamina kumuomba ajiunge na timu Ethiopia ambapo itakuwa ikicheza mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaitta Dicha kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika. “Ambaye alikuwa kocha msaidizi Noel Mwandila amekuwa kaimu kocha mkuu kwa sababu mwalimu hayupo na timu haiwezi kuwa bila kocha mkuu kwa hiyo mkuu wa benchi la ufundi kwa sasa atakuwa Noel Mwandila akisaidiwa na Shadrack Nsajigwa.” “Tumejaribu kumjibu barua ya kujiuzulu lakini pia tumemwandikia kwamba bado tuna nia nae na akaungane na timu Ethiopia lakini bado hatujapata majibu na hatujajua ni kwa sababu gani lakini tumejitahidi hatujapata jibu sahihi.” “Aliwasilisha barua ya kujiuzulu lakini barua lazima ikubal...

MOHAMED SALAH KUJUMUISHWA KWENYE BALLON DO'R,JE UNAJUA NI KWANN ATASHINDA MWAKA HUU?VIGEZO HIVI HAPA

Image
Hakuna kitu kinachotafuna nyoyo za watu kama chuki na unafiki. Walio wengi hawapendi ukweli wa kile wasichokipenda uzidi kudumu. Tukiachilia ushabiki wetu na unazi tulio nao Mo Salah amekuwa na msimu bora kuzidi mchezaji yoyote ndani ya EPL. Ametwa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara 3 na hii inadhihirisha wazi kuwa DALILI YA MVUA NI MAWINGU. Najua roho zinawauma hasa ndugu zangu upande wa pili wanaotokea mashariki mwa Jiji la Liverpool wakipitia mji wa Warrington umbali wa kilometa kama 50 sawa na maili 31 na wale vibaraka wa Mrusi waliomtelekeza. Enewei Kinachonisikitisha zaidi ni kuamini kuwa mchezaji bora lazima timu yake ipate mafanikio. Huu ni uchuro ambao Sepp Blatter ataulizwa na malaika wa Michezo mbinguni. Walio wengi wanaamini ili ubebe Tuzo ya Mchezaji bora wa Dunia lazima timu yako itwae Makombe makubwa kama UCL. Wanasahau Rivaldo alibeba tuzo hiyo na kumwacha nje Andy Cole na Dwight York na Beckham waliobeba makombe manne kwa msimu. Hizi kelele za kigezo cha ...

Man City ndio Bingwa wa EPL msimu 2017/2018

Image
Leo April 15 2018 game ya Man United dhidi ya West Bromwich Albion imethibitisha rasmi kuwa club ya Man City ndio Bingwa wa EPL msimu 2017/2018, hiyo ni baada ya Man United aliyekuwa nafasi ya pili kupoteza mchezo dhidi ya Wets Bromwich leo kwa goli 1-0. Man City wametangazwa kuchukua taji la EPL kwa mara ya tano baada ya wapinzani wao wakuu waliyokuwa wanawafuatia nafasi ya pili Man United kupoteza wakiwa nyumbani, hivyo Man City wametangazwa kuwa Mabingwa kwa kuwa na jumla ya point 87 na wamesalia na michezo mitano, Man City mara ya mwisho kutwaa taji la EPL ilikuwa mwaka 2014. Hivyo Man City ambao wao wamecheza game yao ya EPL wiki hii Jumamosi ya April 14 dhidi ya Tottenham na kushinda magoli 3-1, wanatangazwa Mabingwa kwani hata Man United akishinda game zake zote na Man City akapoteza game zote zilizosalia, Man United atakuwa na point 86 hivyo hakuna club ya EPL inayoweza kufikia point za Man City 87.

Wakili mkuu wa serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka.

Image
Leo April 15, 2018  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli leo April 15, 2018 ameteua Majaji 10 wa Mahakama kuu ya Tanzania na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wakili mkuu wa serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka.

HispaniaCristiano Ronaldo sasa ni wazi kuwa amepata mrithi sahihi katika kazi yake ya soka

Image
Staa wa soka wa kimataifa wa  Ureno  anayeichezea Club ya  Real Madrid  ya  Hispania Cristiano Ronaldo  sasa ni wazi kuwa amepata mrithi sahihi katika kazi yake ya soka  Cristiano Ronaldo Junior ,  Ronaldo JR  ameanza kuchukua headlines akiwa bado ana umri wa miaka 7. Kama hufahamu  Cristiano Ronaldo Junior   ni mtoto wa kwanza wa  Cristiano Ronaldo ana umri wa miaka 7 na sasa ameanza kufuata nyayo za baba yake kwa kuanza kushinda tuzo mbalimbali akiwa bado ana umri wa miaka saba. Ronaldo Junior  April 14 2018 akiwa na bibi yake mzaa baba  Dolores Aveiro  ameshinda tuzo ya kuwa mfungaji bora wa shule baada ya msimu kumalizika, hiyo ni tuzo ya kwanza ya  Ronaldo Junior  kupata katika soka na  Ronaldo  na mama yake wote wamepost katika account zao za instagram kumpongeza  Ronaldo Junior . Kwa upande wa baba mtu mwenyewe  Cristiano Ronaldo  anashikilia rekodi ya kuwa...